ONGEZA UWEZO WAKO WA KUMNYONYESHA MTOTO

 



Mtoto anyonye maziwa ya mama tu hadi ayakapotimiza Miezi sita.
Utakua umemuepushia magonjwa na hatari zingine nyingi tu.

Kama mama hana maziwa ya kutosha mtoto pia anaweza kupewa formula milk ila ni pale tu mama akiwa maefariki au akiwa na tatizo kama hilo la maziwa kuto tosha.

Lakini ni muhimu mama kukazana kuhakikisha maziwa yanatosha ili mtoto awe katika hali salama na afya zaidi.

Fahamu vitu vifuatavyo vimesaidia wengine

Maziwa ya mama yametengenezwa na vtu vi3 vya muhimu

*maji ambayo ndio mengi
*Protein and
*Fats

 Ni muhimu sana kufahamu kwamba  kutoka kwa  Maziwa kunahitaji activity ya hormones/ homoni ziwe stimulated, na kinachostimulate ni mtoto kunyonya au kuvuta chuchu
Hivyo mtoto anavovuta au kunyonya chuchu ya mama yake ndivo hormones za kutengeneza  maziwa zinavozalishwa zaidi, hivyo kuleta matokeo chanya katika unyonyeshaji.

Mama asikate tamaa kumueka mtoto kwenye chuchu hata kama maziwa hayatoki auni machache maana kutasaidia kuzalisha homoni zitakazosaidia kutatua tatizo la maziwa kutotosha.

MLO WA MAMA ANAYENYONYESHA

kupata maji ya kutosha au vyakula vya kimiminika, starch/ wanga (mahindi, viazi
,  ndizi) ya kiasi, protein ( jamii ya kunde, maharage, soya na nyama vyakula vitokanavyo na wanyama) na mafuta ( karanga, mlozi au almond  mbegu za maboga, korosho).

Bila kusahau vyakula vya vitamins and minerals/madini kwa kiasi. (matunda na mboga mboga)

Yaani mlo kamili.

Muweke pia mtoto kwenye chuchu hata kama maziwa hakuna mara kwa mara hii itasaidia uzalishaji wa maziwa.
Ndio mana mama anapotaka kumuachisha mtoto nyonyo hua hampi na maziwa yanakata automatically
So zingatia hilo ikiwezekana uweke timetable ya kufanya hyo therapy kabisa.

*uwatu / fenugreek
Loweka na chemshia kisha kunywa maji yake ya kiwa ya moto au baridi, unaweza weka asali kuongeza ladha.

*Unga wa  mlonge, tumia kama kiungo kwenye vyakula vyako, nyunyizia kijiko full cha chakula on a plate with ready to eat food.
*Pilipili manga kwenye uji anaokunywa mzazi au mtori au chai.
*Mbegu za maboga kama kiungo kwenye chakula au uji unavyopika.

*Maji tena nazidi kuwekea mkazo.

Sample diet
Routine ya kula yenye kuonyesha jinsi utakavyoingizia hzo recepies za kuingeza maziwa kwenye milo yako ya kila siku.

12 asubuh (oat+maziwa+unga wa maboga+ tende) na glass ya maji ya uwatu
2 asubuh chai yako kama kawaida

4 asubuh uji changanya na unga wa maboga + glass ya uwatu

6 /7 lunch yako iwe na protein ya kutosha + glass ya uwatu

Saa 10 maziwa + tende 10

Saa 1/2 ucku dinner na glasss ya uwatu

Saa 4 ucku , saa 6 na saa 9 ucku  either of these, oats+ maziwa+ unga wa maboga+ uwatu.

ZINGATIA
Mama wengi wanaonyonyeaha wanapata stress za kunenepa kupitiliza hivo hawali kama inavotakiwa au wanakua mislead wanakula mno na kujijazia excess mwilini na baadae kujichukia bcoz of mwili kujiachia bila mpangilio.

Kula sana si kupata maziwa mengi. Unatakiwa kula mlo uliokamili na kujitahidi kunyonyesha mtoto wako.

Fanya mazoezi simple ili kuweka mwili wako active na kuzuia unene bila mpangilio


0739904346
0717427302

Comments

Popular posts from this blog

ZIJUE MBEGU ZA UWATU, FAIDA ZAKE NA MATUMIZI.

ROSE WATER MATUMIZI SAHIHI NA FAIDA YAKE.

DETOX YA SIKU 7. HATUA YA KWANZA KUPUNGUZA UNENE