ZIJUE MBEGU ZA UWATU, FAIDA ZAKE NA MATUMIZI.

 


Uwatu (fenugreek) ni mmea wenye asili ya ulaya mashariki na Ethiopia japo unasatawi pia india na Pakistani. Nchini india unajulikana kama methi na unatumika sana katika  katika vyakula mbali mbali na tiba Asilia nchini humo. Kwa hapa Tanzania mmea huu unalimwa Sana pwani visiwa vya unguja na Pemba na unatumika sana katika mapishi ya michuzi, achari na tiba za kisuna

Mmea huu una mbegu za manjano,mbegu zake ni ngumu kwa kushika, zinatumika pia kwenye mapishi ya michuzi, achari, nk pia zinatumika ktk tiba asilia


BAADHI YA FAIDA ZA MBEGU ZA UWATU KIAFYA:-

1. Mbegu hizi zinasaidia kupunguza lehemu (chorestal) mwilini

2. Zinasaidia kuongeza uwingi wa maziwa kwa mama anayenyonyesha.                                              Tia unga wake supu na uji kuongeza kiwango cha maziwa 

3. Zinasaidia kutibu kisukari (diabetes type 2) na pia kurekebisha kiwango cha sukari kwenye damu. 

Loweka kijiko 1 cha chakula cha mbegu za uwatu katika glass moja la maji usiku kucha kisha kunywa 

Note:-                                                                      Utumiaji wa uwatu pamoja na dawa za kisukari zinasababisha low blood pressure hivyo wasiliana na dakatari wako kabla ya matumizi

4. Mbegu hizi zinasemekana kutibu homa na matatizo ya koo kutokana na uwepo wa muciliage.

Tumia mbegu hizi pamoja na kijiko kimoja cha limao na asali kupunguza homa, kuupa nguvu mwili na kuondoa maumivu ya koo.

5. Mbegu za uwatu zinasaidia kuondoa kiungulia kutokana na uwepo wa kiwango kikubwa cha uteute kinachozuia asidi ya tumbo kukutana na kuta tumbo na utumbo

6. Uwatu ni dawa nzuri ya tumbo hasa kwa watoto. Kama tunavyojuia watoto wengi wa kiume huwa wanapata maumivu makali Sana ya tumbo, Chemsha uwatu na maji kisha mpe mtoto yakiwa vugu vugu vijiko 2-3 vya chai atapata utulivu.

7. Inasaidia kutibu maumivu ya tumbo wakati wa hedhi. Ukitumia 1800-2700mg za unga wa uwatu mara tatu kwa siku, kwa zile siku tatu za mwanzo wa hedhi na 900mg mara tatu kwa siku za hedhi zilizobaki kunaondoa maumivu ya tumbo.

8. Mbegu za uwatu ni chazo kikubwa cha vitamins mbali mbali Kama vile, Folic acid, ribloflavin na niacin, vitamin A,vitamin B6 na vitamin c na majani yake yana uwepo wa vitamin K, hivi vyote ni muhimu kwa kinga ya mwili na afya kwa ujumla.

9. Mbegu hizi ni tiba nzuri ya mba kichwani ,twanga mbegu hizi changanya na Maji kidogo kufanya rojo paka kichwani..Mba zitaisha kwa wiki kadhaa au mwezi


Maelezo zaidi whtsap/call 0739904346

Comments

Popular posts from this blog

ROSE WATER MATUMIZI SAHIHI NA FAIDA YAKE.

DETOX YA SIKU 7. HATUA YA KWANZA KUPUNGUZA UNENE