ROSE WATER MATUMIZI SAHIHI NA FAIDA YAKE.
Leo tuzungumzie faida na matumizi ya rose water, Rose water ni maji yaliyotengenezwa kwa kuchuja virutubisho kutoka kwenye maua(petals) ya waridi.
Wengi hupenda maua waridi yanavyonukia basi hutumia rose water kwa ajili ya aroma therapy, yaani kurelax huku ukisikiliza harufu nzuri inayotuliza akili.
Matumizi ya rose water mengine ni kama ifuatavyo;
Toner
Rose water inaweza kutumika kutone ngozi yako maana insaidia kupunguza bakteria katika ngozi yako hivyo pia husaidia kuondoa chunusi, inasaidia kuondoa muonekano wa ngozi kuwa na alergy mfano wekundu wa ngozi kwa watu weupe n.k wakati huo huo huipa ngozi yako unyevu na kuituliza ngozi yako. Ukimaliza kusafisha uso wako chukua pamba kidogo iweke rose water na kisha jifute/ paka usoni iwapo una wekundu unaotokana na inflamation(alergy/muitikio wa ngozi) utaona unapotea.
Tunapoongelea toning ni kama hivi, yaani ngozi yako inaenda inalingana na kupata mng'ao
Make Up remover ( Kuondoa Make up)
Rose water inasafisha ngozi vizuri unapojifuta na pamba hivyo hata uwe umepaka make up ya kugandia huwa inaondoshwa na rosewater unapofuta. Haya maji huweza kuondoa hata make up zinazoandikwa water proof kama mascara au eye shadow na kuiacha ngozi yako ikiwa na unyevu.
Katika kufanya macho yako yaonekane vizuri
Rose water inasidia kupunguza dark cycles na ile hali ya jicho kuvimba (baggy Eyes) kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kukosa kulala usingizi vizuri. ukichukua pamba yako iliyochovya kwenye rose water itumie kufuta taratibu au kukanda kwa mbali kuzunguka jicho lako baada ya muda jicho linakuwa powa.
Dark Cycle
Kuupa uso wako uhai pale make up yako inapofifia
Iwapo umepaka make up inapooza au kutokana na joto uso unachemka, basi kuwa na kichupa kidogo unachoweka rose water ambayo utaweza kuspray uson pako, uso unachangamka. Pia kama unapata joto sana usoni unaweza kutumia pamba kidogo yenye rose water hivyo kuupooza.
Unaweza Kuiongezea katika treatment ya uso
Iwapo wewe ni muumini wa natural treatment kama ya kupaka manjano usoni basi badala ya kuchanganyia maji unaweza kuchanganya na rose water kisha unapaka usoni kama inavoonekana katika picha.
Kurelax mwili na akili
Unaweza kuweka rose water katika maji unayoogea ili kuipata ile harufu murua wakati ukioga. Hii inatuliza akili na kukufanya urelax.
Pia Unaweza kuitia katika mashuka yako yawe na harufu nzuri kwa kuspray kabla hujayatandika au ukianika yanapokaribia kukauka.
Ushauri zaid usisite kuwasiliana nasi 0739904346
Comments
Post a Comment