DETOX YA SIKU 7. HATUA YA KWANZA KUPUNGUZA UNENE

 

HATUA YA KWANZA KUPUNGUZA UNENE.



Uzito Unaotakiwa kua nao Kulingana na Urefu Pamoja na Jinsia

UREFU (CM)

UREFU (FT & INCH)

UZITO (KG)

 

 

 

MWANAUME

MWANAMKE

147

4' 10"

-

45-59

150

4' 11"

-

45-60

152

5' 0"

-

46-62

155

5' 1"

55-66

47-63

157

5' 2"

56-67

49-65

160

5' 3"

57-68

50-67

162

5' 4"

58-70

51-69

165

5' 5"

59-72

53-70

167

5' 6"

60-74

54-72

170

5' 7"

61-75

55-74

172

5' 8"

62-77

57-75

175

5' 9"

63-79

58-77

177

5' 10"

64-81

60-78

180

5' 11"

65-83

61-80

182

6' 0"

66-85

-

185

6' 1"

68-87

-

187

6' 2"

69-89

-

190

6' 3"

71-91

-


MAMBO YA KUFANYA KABLA YA KUANZA DETOX

  •          Jua kwanza uzito wako
  •          Weka malengo ya uzito unaotaka kuufikia (hii itakusaidia kutokukata tamaa)
  •          Ondoa vitu vyote vitakavyokushawishi kuharibu Diet yako na ujiepushe katika mazingira hayo.
  •          Fanya maandalizi ya vitu utakavyovihitaji kwa kila siku, hii itakusaidia kutokua na visingizio vya kutokufwata ratiba. KUSHINDWA KUJIANDAA NI KUJIANDAAKUSHINDWA.
  •          Nunua Tape measure ili uwe unajipima cm za tumbo lako kuweza kujua maendeleo yako, utakua ukifanya hivi kila siku ya 7 ya wiki. Unaweza pia kua na mzani utakaotumia kama ukiweza.
  •          Chukia unene kutoka ndani ya moyo, fikiria madhara yote yanayotokana na unene na ujue kabisa umri unavyozidi kwenda una chance kubwa za kupatwa na athari hizo. Na kisha fikiria mwili wako utakavyokua endapo ukiwa na uzito sahihi

Mabadiliko Utakayokua nayo Ukiweka Nia kwa Miezi 6

PROGRAMU YA DETOX (D7)

Nini maana ya Detox?

DETOX ni kifupisho cha neno DETOXIFICATIONikiwa na maana ya mchakato au kipindi cha muda flani ambacho mtu hujizuia kuingiza mwilini ama kuondoa dutu (substances) zenye sumu mwilini au ambazo hazina faida kiafya.

KUNA FAIDA GANI KUFANYA DETOX?

  •   Kupunguza uzito uliozidi na kua na mmeng'enyo mzuri wa chakula
  •   Kuongeza nguvu katika mwili. (boost energy levels)
  •   Kupunguza uchochezi (inflammation)
  •   Kua na ngozi yenye afya
  •   Kuongeza kinga ya mwili
  •   Kuamsha ari (mood) au kua mchangamfu.

DALILI ZINAZOASHIRIA KUA MWILI UNAHITAJI DETOX

  •   Kuongezeka uzito
  •   Kua na hamu ya kula hovyo na kupenda sana vitu vya sukari
  •   Kuchoka mara kwa mara
  •   Kutokupata usingizi wakati wa usiku
  •   Kupungua kwa ufanisi wa kufikiri
  •   Maumivu ya kichwa mara kwa mara
  •   Kubadilika kwa mihemko mara kwa mara (mood swings)
  •   Harufu mbaya ya kinywa na maeneo mengine
  •   Kukosa choo au kupata choo kigumu
  •   Maumivu ya misuli
  •   Matatizo ya ngozi (skin reactions)

JINSI YA KUANDAA DETOX

Hapa tutakua na aina 2 za detox.

Detox type 1 ambayo ni mchanganyiko wa tango, limao, mdalasini, tangawizi pamoja na majani ya mint.

Pamoja na detox type 2, ambayo ni supu ya kabichi.

Hapa utakua na uhuru wa kutumia yoyote unayoona ni rahisi kwako na zote ukapata matokeo mazuri.

Uamuzi ni wa kwako, kua huru kutumia aina yoyote unayopenda.

Lakini kwa wale ambao wana vidonda vya tumbo, nawashauri kutumia Detox type 2. Kwani haina vile vitu ambavyo wagonjwa wa vidonda vya tumbo hua wanashauriwa wasitumie.

DETOX TYPE 1.

Andaa vitu vifwatavyo;

  •   Tango 1 kubwa
  •   Limao 1 kubwa au ndimu
  •   Mdalasini kipande 1 kikubwa (kama ni ya unga basi tumia kijiko 1 cha chakula)
  •   Tangawizi 1 kubwa, kisha iponde au kata vipande vidogo.
  •   Majani ya mint kiasi cha nusu kikombe. Au ukikosa majani ya mint tumia majani ya giligilani (kotmil kwa jina jingine au coriander kwa kingereza). (Mint kwa kiswahili ni majani ya Nanaa)
  •   Maji lita 1.






JINSI YA KUTENGENEZA DETOX YAKO

  •   Kata tango lako katika vipande vya mviringo au vipande vidogo kisha weka kwenye blenda yako. (usilimenye, ila hakikisha umeosha vizuri).
  •   Kamulia limao/ndimu yako (usije ukasaga na maganda yake au mbegu, bali kamulia)
  •   Weka mdalasini, tangawizi na majani ya mint/giligilani kwenye mchanganyiko wako.
  •   Saga hadi utakapopata mchanganyiko wako ambao umelainika. (hakikisha unasaga hadi vilainike)
  •   Mchanganyiko utakaoupata, hifadhi kwenye friji. (kama una friji, unaweza kutengeneza hata mchanganyiko wako wa wiki nzima)
  •   Kama huna friji, hifadhi sehemu ambayo imetulia. Ila usitengeneze ya kutumia Zaidi ya siku mbili, kwani isipokaa kwenye friji mda mrefu inachacha.

KAMA HUNA BLENDA FANYA HIVI;

  •   Kata tango lako katika vipande vya mviringo (slices) kisha weka kwenye  jagi lenye maji (usilimenye, ila hakikisha umeosha vizuri)
  •   Kata limao/ndimu yako katika vipande vya mviringo (slices) na kisha uweke kwenye lile jagi lenye maji (pia usimenye, ila hakikisha umeosha vizuri)
  •   Weka mdalasini, tangawizi na majani ya mint kwenye jagi (vipimo kama nilivyoeleza awali)
  •   Weka sehemu iliyotulia na uhifadhi kwa usiku mzima. Au muda usiopungua masaa 2
  • Ø  Kisha utakapoamka asubuhi, (au baada ya masaa 2) detox yako itakua tayari kwa matumizi. Yale mabaki unaweza kuyatumia kwa kula au ukayatupa, ila usitumie yale mabaki mara ya 2, inatakiwa iwe mara moja tu.

DETOX TYPE 2

Andaa vifuatavyo;

  •   Kabichi nusu
  •   Kitunguu maji 1
  •   Pili pili hoho 1
  •   Kitunguu swaumu 1
  •   Nyanya 3
  •   Karoti 3
  •   Chumvi
  •   Pilipili manga au pilipili kiasi (kama sio mtumiaji wa pilipili sio lazima)
  •   Viungo vingine vyovyote kulingana na uhitaji.

JINSI YA KUTENGENEZA DETOX YAKO

  •   Likate kabichi lako katika vipande ambayo umezoea.
  •   Kata kitunguu maji pamoja na pilipili hoho.
  •   Ponda kifundo kimoja cha kitunguu swaumu.
  •   Kata nyanya zako au ponda kulingana na ulivyozoea. (nyanya sio lazima kutumia kama hupendelei)
  •   Kata karoti zako 3 katika mtindo unaopendelea.
  •   Weka chumvi, pili pili manga au pilipili, (kama hupendi pilipili sio lazima). Unaweza kuongezea na viungo vingine ukipenda.

IPIKE HIVI

  •   Kaanga mboga mboga (zilizotajwa hapo juu) pamoja na kitunguu (kabla ya kuweka kabichi na nyanya). Kaanga hadi kitunguu kibadilike rangi lakini usiunguze
  •   Kisha weka kabichi na nyanya pamoja na maji hadi vichemke na kabichi kulainika na kuiva.
  •   Baada ya kuiva, epua na sasa inakua tayari kwa matumizi. Unaweza kuhifadhi kwenye chupa ya chai (thermos) ili uweze kuhifadhi na kutumia mda wowote ule.

UNAWEZA KUIFANYA KAMA MTORI UKIPENDA;

  •   Kama kuna supu yoyote ile, yaweza kua ya ng'ombe, mbuzi, samaki, kuku n.k. chukua ile supu yake na kisha ukasaga pamoja na ile supu yako ya kabichi. Na kisha ukatumia mchanganyiko utakaopata.
  •   Au unaweza kuchukua supu yako ya kabichi uliyotengeneza na kisha ukasaga kupata mtori wa supu ya kabichi na ukatumia vizuri tu bila shida

JINSI YA KULA KATIKA SIKU 7 ZA DETOX.

Kabla ya kuelezea jinsi ya kula katika siku hizi 7. Ifahamike ya kwamba lengo la detox sio diet. Lengo la detox ni kuandaa mwili wako ili uweze kuingia hatika hatua ya kupungua uzito na kupokea virutubisho.

Hivyo mtindo huu wa kula usiutumie Zaidi ya siku saba. Unatakiwa kutumika kwa siku 7 TU.

Ifahamike ya kwamba, katika siku yoyote, asubuhi kabla ya kula chochote unaanza na glass moja ya detox type 1, au bakuli moja la detox type 2. (ni uamuzi wako kutumia kati ya type 1 au type 2.

Hivyo kama unatumia type 1. Utakua ukitumia glass 1 asubuhi, glass moja mchana na glass moja jioni. (hivyo utaanza na detox yako, ndipo ule kulingana na ratiba iliyopangwa)

Na kama unatumia type 2. Utakua ukitumia bakuli 1 asubuhi, bakuli 1 mchana na bakuli 1 jioni. (hivyo utaanza kunywa detox soup yako ndipo ule kulingana na ratiba ya siku husika)

Vyakula hivi unaweza kupika na kuunga kwa mtindo wowote ule ambao unapendelea. (ila jitahidi kutokutumia chumvi nyingi na mafuta mengi)

JINSI YA KULA KATIKA SIKU 7 ZA DETOX

SIKU YA 1

Tumia matunda peke yake. Unaweza kuchanganya matunda yoyote unayopenda asubuhi, mchana pamoja na jioni. Hapa utakula matunda mpaka pale utakapojihisi umeshiba.

SIKU YA 2

Tumia mboga mboga tu. Kula mpaka utakapohisi umeshiba. Utafanya hivyo asubuhi mchana na jioni. Mfano maboga, spinachi, mchicha, matembele, bilinganya na chochote kile ambacho kipo katika kundi la mboga mboga.

SIKU YA 3

Tumia mboga mboga pamoja na matunda mpaka utakapohisi shibe. Unaweza kuchanganya katika mtindo wowote ule, ilimradi iwe ni mboga mboga pamoja na matunda.

SIKU YA 4

Tumia matunda pamoja na maziwa. Yanaweza kua maziwa fresh au ya mtindi hadi lita moja na nusu kwa siku. (usizidishe lita moja na nusu).

 

Ikiwa hupendelei au hutumii maziwa, basi mbadala wake ni mayai. Yanaweza kua mawili kwa kila mlo.

SIKU YA 5

Tumia nyama pamoja na nyanya walau 3 hadi 5. Nyama inaweza kua ya kuchoma au kuchemsha. Ila usizidishe Zaidi ya nusu kilo kwa siku. Nyama yaweza kua ya ng'ombe, mbuzi, kuku, samaki n.k

Kama sio mtumiaji wa nyama, unaweza kutumia vyanzo vingine vya protini kama vile maharage, njegere, mbaazi, njugumawe, choroko pamoja na kunde.

 

NB; napendekeza Zaidi protini inayotokana na mimea kuliko za wanyama. Kwwa sabau mimea ina virutubisho vingi Zaidi (phytonutrients) wakati nyama hazina phytonutrients.

SIKU YA 6

Tumia protini itokanazo na mimea (kama nilivyotaja hapo juu) pamoja na mboga mboga zozote hadi uhisi umeshiba.

 

Mbadala wake unaweza kutumia nyama ya kuchoma au kuchemsha pamoja na mboga mboga.

SIKU YA 7

Tumia wanga mzuri kama vile viazi vitamu, ugali wa dona au wa mtama, magimbi au boga. Tumia viazi vitamu 2 pamoja na mboga mboga zozote.



NB: siku ya 1 na ya 2 zinaweza kua na changamoto. Kwani ndio unautoa mwili wako kutoka kwenye ulaji mbaya na usiofaa kwenda kwenye ulaji mzuri. Hivyo wakati mwili wako unafanya mabadiliko hayo, huenda ukasikia ugumu kwa siku ya 1 na ya 2. Lakini kuanzia siku ya 3, mwili wako utakua umezoea na utaanza kujihisi mwepesi sana.

MAMBO YA KUZINGATIA

  •   Usisahau kutumia ile detox yako (type 1 au type 2) kila siku. Asubuhi mchana na jioni.
  •   Kunywa maji mengi kadri uwezavyo, kwani maji yanasaidia katika kusafisha mwili.
  •   Kwa kua program hii ni maalum, jitahidi usikiuke mwongozo kwa siku 7 ili uweze kupata matokeo mazuri.
  •   Punguza matumizi ya pombe (ikiwezekana usitumie wakati wa D7)
  •   Pata usingizi wa kutosha. (angalau masaa 8 kwa siku)
  •   Punguza matumizi ya sukari na vyakula vya viwandani
  •   Punguza matumizi ya chumvi
  •   Shughulisha mwili, tembea (jambo rahisi kabisa), fanya mazoezi, ruka Kamba, endesha baiskeli (walau nusu saa kwa siku)

NINI KITATOKEA BAADA YA DETOX?

  •   Utajisikia mwepesi sana kwa sababu ya kuweza kutoa taka mwili
  •   Utapungua uzito au kitambi, kama nguo zilikua zinakubana, basi utaona zinaanza kukutosha au kupwaya. Au kama unavaa mkanda basi utaona ni lazima uongeze tundu jingine ili uweze kukutosha.
  •   Utapungua wastani wa kilo 3 mpaka 7 ndani ya siku 7 (hii inategemea na mwili wa mtu. Hivyo ikitokea umepungua chache wala usishtuke)
  •   Utapoteza hamu ya kula vyakula visivyo na faida kama vile soda, vyakula vya sukari n.k
  •   Wakati wa detox, utaona ya kwamba unakojoa sana. Hii ni hali ya kawaida kwani figo zako sasa zinafanya kazi kwa ufanisi. Kitaalam kuna kitu tunaita WATER RETENTION. Hii ni hali ambayo maji yanabaki ndani ya mwili badala ya kutoka. Hali hii husababishwa sana na ulaji mbovu na utumiaji wa chumvi nyingi. Hii hupelekea maji mengi kubaki mwilini badala ya kutoka. Na kama inavyofahamika, maji hua yana uzito, hivyo yanapobaki mwilini yanachangia kwa kiasi kikubwa kua na uzito mkubwa. Hivyo ukiona unakojoa sana, ni hali ya kawaida.

 NINI CHA KUFANYA ENDAPO UTAHISI NJAA KALI WAKATI WA DETOX

Hapa utatumia vyakula vifwatavyo ili usishinde na njaa. Kumbuka kua detox ni kwa ajili ya kusafisha mwili wako, lakini usikubali kushinda na njaa.

  •          Gimbi
  •          Kiazi kitamu
  •          Uji wa ulezi
  •          Uji wa oats
  •          Ugali wa dona/uji wa dona
  •          Wali wa brown
  •          Mhindi
  •          Uji/ugali wa mtama
  •          Bagia za dengu au kunde
  •          Maharage, njegere, choroko, kunde au dengu.

Orodha hii ni vyakula vya wanga mzuri. Kama ukiona sjaandika kitu flani, basi ujue sio rafiki kwa detox, hata kama ni wanga.

Kipimo ni cha ukubwa wa ngumi au kipimo cha bakuli 1 kwa wanga wa kumiminikakama vile uji.


 IKIWA UNANYONYESHA MTOTO ZAIDI YA MIEZI 3

Tumia vyakula hivi ili upate maziwa mengi ya kutosha kwa mtoto huku ukiendelea na programu. Kama mtoto ana chini ya umri wa miezi 3, nashauri usubiri kwanza atomize miez 3.

  •          Spinachi
  •          Karoti
  •          Papai
  •          Mayai
  •          Parachichi
  •          Samaki
  •          Boga
  •          Maziwa
  •          Vitunguu swaumu
  •          Wali wa brown
  •          Uji wa oats au oats meal
  •          Kiazi kitamu

 ANGALIZO

  •   Usifanye detox hii Zaidi ya siku 7. Kumbuka kua detox ni kwa ajili ya kuandaa mwili wako uweze kupokea virutubisho ili uweze kupungua kwa urahisi. Ukizidisha unaweza kupata hormonal imbalance. Baada ya siku 7, kuna mwongozo mwingine.
  •   Kama ni mjamzito. Hutakiwi kutumia detox au program yoyote ya kupungua uzito. Na kama unanyonyesha, basi mtoto awe na umri wa kuanzia miezi 3 au Zaidi.
  •   Kama unaumwa au upo kwenye dozi. Nakushauri usitumie detox, ni vyema ukasubiri upone. Labda kama upo kwenye dozi za muda mrefu mf kisukari, presha n.k ndo unaweza kutumia

NB; ENDAPO UTAZINGATIA MWONGOZO HUU KAMA NILIVYOELEZA, NINAKUHAKIKISHIA YA KWAMBA UTAPATA MATOKEO MAZURI MNO. NA SAFARI YAKO YA KUPUNGUA NDO ITAKUA IMEANZA SASA RASMI.

CHUKUA HATUA, UNENE SIO MZURI HATA KIDOGO.

 KARIBU KATIKA ULIMWENGU WA AFYA 

Comments

Popular posts from this blog

ZIJUE MBEGU ZA UWATU, FAIDA ZAKE NA MATUMIZI.

ROSE WATER MATUMIZI SAHIHI NA FAIDA YAKE.