Posts

Showing posts from October, 2021

ONGEZA UWEZO WAKO WA KUMNYONYESHA MTOTO

Image
  Mtoto anyonye maziwa ya mama tu hadi ayakapotimiza Miezi sita. Utakua umemuepushia magonjwa na hatari zingine nyingi tu. Kama mama hana maziwa ya kutosha mtoto pia anaweza kupewa formula milk ila ni pale tu mama akiwa maefariki au akiwa na tatizo kama hilo la maziwa kuto tosha. Lakini ni muhimu mama kukazana kuhakikisha maziwa yanatosha ili mtoto awe katika hali salama na afya zaidi. Fahamu vitu vifuatavyo vimesaidia wengine Maziwa ya mama yametengenezwa na vtu vi3 vya muhimu *maji ambayo ndio mengi *Protein and *Fats  Ni muhimu sana kufahamu kwamba  kutoka kwa  Maziwa kunahitaji activity ya hormones/ homoni ziwe stimulated, na kinachostimulate ni mtoto kunyonya au kuvuta chuchu Hivyo mtoto anavovuta au kunyonya chuchu ya mama yake ndivo hormones za kutengeneza  maziwa zinavozalishwa zaidi, hivyo kuleta matokeo chanya katika unyonyeshaji. Mama asikate tamaa kumueka mtoto kwenye chuchu hata kama maziwa hayatoki auni machache maana kutasaidia kuzalisha homoni zitakazosaidia kutatua tat

Matumizi Ya Maganda Ya Machungwa Katika Urembo

Image
  1. Maganda ya machungwa kutoa vinyweleo usoni  Maganda ya machungwa huondoa  vinyweleo usoni Wanawake wengi hulala-mikia tatizo la kutokwa na vinyweleo vingi kwenye miili yao. Wengine hutumia mbinu ya kuvinyoa kwa kutumia wembe ambapo badala ya kuvipunguza, husababisha viongezeke na ngozi za nyuso zao kuzeeka. Badala ya kutumia krimu kali au wembe,  maganda ya machungwa Unga wa maganda ya machungwa au malimao kijiko kimoja. Unaweza kuandaa unga huo kwa kuyakausha maganda hayo juani kwa siku kadhaa kisha ukayatwanga na kuyasaga kupata ungaunga wake. Vijiko viwili vya mafuta ya mzaituni (olive oil). Kijiko kimoja cha unga wa mtama.                      Kijiko kimoja cha maji ya waridi (rose water).             Namna Ya Kuandaa                 Changanya unga wa maganda ya machungwa au malimao na unga wa mtama kwenye chombo kimoja kisha ongeza mafuta ya mzaituni pamoja na maji ya waridi. Changanya mpaka upate ujiuji mzito. Jipake ujiuji huo usoni na uache ukae kwa dakika kumi. Baada ya h

ZIJUE MBEGU ZA UWATU, FAIDA ZAKE NA MATUMIZI.

Image
  Uwatu (fenugreek) ni mmea wenye asili ya ulaya mashariki na Ethiopia japo unasatawi pia india na Pakistani. Nchini india unajulikana kama methi na unatumika sana katika  katika vyakula mbali mbali na tiba Asilia nchini humo. Kwa hapa Tanzania mmea huu unalimwa Sana pwani visiwa vya unguja na Pemba na unatumika sana katika mapishi ya michuzi, achari na tiba za kisuna Mmea huu una mbegu za manjano,mbegu zake ni ngumu kwa kushika, zinatumika pia kwenye mapishi ya michuzi, achari, nk pia zinatumika ktk tiba asilia BAADHI YA FAIDA ZA MBEGU ZA UWATU KIAFYA:- 1. Mbegu hizi zinasaidia kupunguza lehemu (chorestal) mwilini 2. Zinasaidia kuongeza uwingi wa maziwa kwa mama anayenyonyesha.                                              Tia unga wake supu na uji kuongeza kiwango cha maziwa  3. Zinasaidia kutibu kisukari (diabetes type 2) na pia kurekebisha kiwango cha sukari kwenye damu.  Loweka kijiko 1 cha chakula cha mbegu za uwatu katika glass moja la maji usiku kucha kisha kunywa  Note:-       

ROSE WATER MATUMIZI SAHIHI NA FAIDA YAKE.

Image
Leo tuzungumzie faida na matumizi ya rose water, Rose water ni maji yaliyotengenezwa kwa kuchuja virutubisho kutoka kwenye maua(petals) ya waridi. Wengi hupenda maua waridi yanavyonukia basi hutumia rose water kwa ajili ya aroma therapy, yaani kurelax huku ukisikiliza harufu nzuri inayotuliza akili. Matumizi ya rose water mengine ni kama ifuatavyo; Toner Rose water inaweza kutumika kutone ngozi yako maana insaidia kupunguza bakteria katika ngozi yako hivyo pia husaidia kuondoa chunusi, inasaidia kuondoa muonekano wa ngozi kuwa na alergy mfano wekundu wa ngozi kwa watu weupe n.k wakati huo huo huipa ngozi yako unyevu na kuituliza ngozi yako. Ukimaliza kusafisha uso wako chukua pamba kidogo iweke rose water na kisha jifute/ paka usoni iwapo una wekundu unaotokana na inflamation(alergy/muitikio wa ngozi) utaona unapotea. Tunapoongelea toning ni kama hivi, yaani ngozi yako inaenda inalingana na kupata mng'ao Make Up remover ( Kuondoa Make up) Rose water inasafisha ngozi vizuri unapojif